MASHEHA WA MKOA WA KASKAZINI UNGUJA WAPATIWA ELIMU YA DIASPORA

  • Nov 15, 2016
  • 149 Views

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja ndugu Vuai Mwinyi Khamis amewataka masheha wa Mkoa huo kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi wao kutambua juu ya nafasi ya mchango waliokuwa nao wazanzibari wanaoishi nchi za nje katika kuchangia miradi mbali mbali ya kiuchumi na kijamii katika nchi yao.

Alisema bado dhana ya diaspora kwa wananchi waliowengi hasa sehemu za vijijini bado haijafahamika vilivyo kwa wananchi hivyo ni vyema kwa masheha wakaitumia vizuri elimu wanayakuwa wanaipata juu ya nafasi waliyokuwa nayo waznaizbrai katika kuchagia maendeleo wakaifikisha kwa wananchi wao.

Nd. Vuai ameyaeleza hayo leo jana katika Hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kaskazini `A` Bw. Mohd Omar wakati alipokuwa akizugumza katika ufunguzi wa semina iliyoahusisha masheha wa Mkoa wa Kaskazini Unguja huko katika ukumbi wa Chuo cha Mafunzo ya Amali Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja. 

Alisema anaamini kuwa elimu waliyoipata masheha hao itatoa elimu itakayowafahamisha namna Wazanzibari walioko nje ya nchi walivyokuwa na nafasi ya kuzitumia harakati zao bila ya kusahau kuchangia maendeleo katika sekta mbali mbali za kichumi na kijamii hivyo kusukuma maendeleo ya nchi yao. `Naamini kuwafikia elimu hii nyinyi masheha itakuwa dira ya kurudi katikamaeneo yenu kusambaza elimu hii ya umuhimu wa kuanzishwa kitengo cha Dispora ambacho kiimarika kwake na kutambulika kwake ndio faida ya jamii ya Wazanzibari wote`alisema Mkuu huyo wa Mkoa. 

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa wa Kaskazini Unguja ameipongeza Idara ya Ushirikiano waKimataifa na Wazanzibari wanaoishi nchi za nje kwa juhudi kubwa wanazozitoa za kutoa elimu kwa viongozi na wananchi kuwaelimisha nafasi na fursa walizokuwa nazo wananchi hao katika kuchangia harakati za Maendeleo. ` Kwa hakika hii Idara inafanya kazi zake vizuri sote tunastahiki kuiunga mkono ili iweze kufanikisha malengo yake kwa maslahi ya jamii yetu na taifa kwa jumla` alisema.

Mapema Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiani waWazanzibari wanaoishi nje ya nchi Adila Hilal Vuai amesema Idara yake mbali ya kuwa na jukumu la kuwashajiisha jamii ya Wazanzibar walioko nje ya nchi kusaidia harakati za maendeleo katika nchi zao lakini wamekuwa na utaratibu wa kutoa elimu kwa wananchi wa mjini na vijiji kutambua uwepo wa Idara hiyo, umuhimu wake na mchango wa wazanzibari walioko nje ya nchi walivyokuwa na fursa ya kuchangia maendeleo ya Taifa letu. 

Alisema Idara yake inajiweka karibu na masheha pamoja na jumuia za kiraia ili kuwa kiungo muhimu katika ngazi za Shehia na vijiji ambavyo wanadispora wengi wamekuwa wakitokea sehemu hizo ambazo faida za michango yao pia itaweza kuwafikia huko. `Ndugu zetu hao mbali ya nafasi waliyokuwa nayo ya kujisaidiawao katika harakati zao za maisha na familia zao lakini pia wanayo nafasiki kubwa ya kuchangia maendelea ya kijamii ambayo kazi hiyo tayari wameshaanza kuianza ndugu zetu hao walioko nje ya nje` alisema Mkurugenzi Adila. 

Semina hiyo iliyotayarishwa na Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Wazanzibari walioko nje ya nchi imezungumzia mada mbili muhimu moja ikiwemo mada ya Diaspora na Maendeleo Zanzibar iliyotolewa na Ali Ameir Hajina ambayo ilichambua Dhana ya Diaspora ni umuhimu wake kwa Zanzibar na fursa za maendeleo zinazopatikana katika Jumuia ya Afrika Mashariki nafasi ya Zanzibar katika utekelezaji wa Soko la Pamoja la Jumuia ya Afrika Mashariki iliyotolewa na Afisa kutoka Kitengo hicho Suleiman Muhsin Haji.

Afisa kutoka Kitengo cha Diaspora Haji Ameir Haji akiwasilisha mada inayohusiana na dhana ya Diaspora na Maendeleo Zanzizbar.
Afisa kutoka Kitengo cha Diaspora Haji Ameir Haji akiwasilisha mada inayohusiana na dhana ya Diaspora na Maendeleo Zanzizbar.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kaskazini `A` Bw. Mohd O. Hamad katika picha ya pamoja na msheha baada ya ufunguzi wa semina hiyo.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kaskazini `A` Bw. Mohd O. Hamad katika picha ya pamoja na msheha baada ya ufunguzi wa semina hiyo.

Related Articles