Idara hii inahusika na masuala ya uratibu wa Ushiriki wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika shughuli za Kikanda na Kimataifa katika nyanja za kiuchumi, kijamii; pamoja na uratibu wa shughuli za Wazanzibari Wanaoishi Nje ya Nchi na kuhakikisha wanahusishwa kikamilifu katika Maendeleo ya Zanzibar.
Majukumu
1. Kuimarisha mtangamano wa Kikanda ili kuweza kutumia fursa za kiuchumi zinazotokana na Jumuiya za Kikanda.
2. Kusimamia uimarishaji wa ushirikiano mwema na nchi marafiki na Taasisi za Kimataifa;
3. Kuwashajihisha na kuwashirikisha Wazanzibari Wanaoishi Nje ya Nchi kushiriki katika shughuli za imaendeleo ya kijamii na kiuchumi; na
4. Kuratibu masuala ya Itifaki ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi