JUMUIA YA AHAS GROUPS YATOA VIFAA VYA SKULI NA HOSPITALI UNGUJA.

  • Apr 10, 2019
  • 165 Views

umuia ya Wazanzibari wanaoishi nchini Dermark ya ‘AHAS GROUP’ mapema mwezi wa April 2019 iliendelea na utaratibu wake wa utoaji wa msaada wa vifaa kwa Skuli ya Sekondari ya Kidongo Chekundu, Hospitali ya Mnazi Mmoja zilizopo Wilaya ya Mjini na Hospitali ya Cottage ya Kivunge iliyoko Mkoa wa Kaskazini Unguja Wilaya ya Kaskazini “A” kwa ajili ya kuimarisha huduma za kijamii.

Jumuia ya Wazanzibari wanaoishi nchini Dermark ya ‘AHAS GROUP’ mapema mwezi wa April 2019 iliendelea na utaratibu wake wa utoaji wa msaada wa vifaa kwa Skuli ya Sekondari ya Kidongo Chekundu, Hospitali ya Mnazi Mmoja zilizopo Wilaya ya Mjini na Hospitali ya Cottage ya Kivunge iliyoko Mkoa wa Kaskazini Unguja Wilaya ya Kaskazini “A” kwa ajili ya kuimarisha huduma za kijamii.

Vifaa hivyo vilitolewa kwa wahusika kwa nyakati tofauti na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Uratibu wa Wazanzibari wanaoishi nje ya nchi Ndugu Adila Hilal Vuai akiwa na Mwakilishi wa Jumuia ya Ahas Group Bw. Ali Talib.

Mkurugenzi Adila amezihimiza jumuiya nyengine za Wazanzibari zilizoko nchi mbali mbali kuongeza ushirikiano na Idara yake hasa katika masuala ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii kupitia misaada na taaluma inayotokana na jumua zao.

Vifaa vilivyotolewa kwa upande wa skuli ya Sekondari ya Kidongo Chekundu ni pamoja na meza, viti, kompyuta na baiskeli na Hospitali ya Mnazi mmoja ilipokea vifaa vya kuchezea kwa ajili ya wodi ya watoto, aidha vitanda vinne vilitolewa kwa Hospitali ya Cottage ya Kivunge kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wenye matatizo ya mgongo.

Wahusika wote hao waliokabidhiwa vifaa hivyo wameipongeza na kuishukuru Jumuia ya Ahas Group kutokana na juhudi zake inazozichukua hasa zinazohusiana na sekta za kijamii zikiwemo za elimu na afya. pia waliipongeza Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Uratibu wa Wazanzibari wanaoishi nje ya nchi kwa kuendelea kuwa nao bega kwa bega katika kuwashajihisha kuunga mkono juhudi za maendeleo nchini.

Related Articles