Waziri wa nchi ofisi ya rais ikulu Dkt Saada Salum Mkuya amesema kuwa Uzinduzi wa Mfumo wa Usajili wa Diaspora wa Zanzibar ni hatua ya kimkakati ya Serikali katika kupanga, kuratibu na kuongeza tija

  • Jan 20, 2026
  • 2 Views

Waziri wa nchi ofisi ya rais ikulu Dkt  Saada Salum Mkuya amesema kuwa Uzinduzi wa Mfumo wa Usajili wa Diaspora wa Zanzibar ni hatua ya kimkakati ya Serikali katika kupanga, kuratibu na kuongeza tija ya mchango wa Diaspora katika maendeleo ya Taifa. Ameyasema hayo leo 21/01/2026 katika uzinduzi wa mfumo wa usajili  diaspora wenye asili ya Zanzibar  huko verde wilaya ya magharibi ,amesema kupitia mfumo huu, Serikali itapata takwimu sahihi zitakazowezesha kuwaunganisha Wanadiaspora na fursa za uwekezaji katika sekta za kipaumbele ikiwemo utalii, uchumi wa buluu, kilimo, afya, elimu, TEHAMA na viwanda vidogo. ni hatua ya kimkakati ya Serikali katika kupanga, kuratibu na kuongeza tija ya mchango wa Diaspora katika maendeleo ya Taifa. Ameyasema hayo leo 21/01/2026 katika uzinduzi wa mfumo wa usajili  diaspora wenye asili ya Zanzibar  huko verde wilaya ya magharibi ,amesema kupitia mfumo huu, Serikali itapata takwimu sahihi zitakazowezesha kuwaunganisha Wanadiaspora na fursa za uwekezaji katika sekta za kipaumbele ikiwemo utalii, uchumi wa buluu, kilimo, afya, elimu, TEHAMA na viwanda vidogo.

Dkt Saada amesema kuwa Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji, kuimarisha sera na mifumo ya uwazi, ili kuhakikisha kuwa kila Mzanzibari aliyeko nje anaona thamani na usalama wa kuwekeza nyumbani. Pia Dkt Saada ameeleza kuwa Mfumo huu unaonesha dhamira ya Serikali ya kutumia teknolojia ya kidijitali kama nyenzo muhimu ya utekelezaji wa Sera, utoaji wa huduma, na usimamizi wa rasilimali watu kwa Maendeleo ya Taifa.

Aidha ameeleza kuwa mfumo huo  kikamilifu unaendelea na Dira ya Maendeleo ya Zanzibar 2050, Agenda 2063 ya Umoja wa Afrika, pamoja na Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), hususan SDG 8, 9 na 17.

Nae Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu Ndg Saleh Juma   Mussa amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, chini ya uongozi wa  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, dkt Hussein ali mwinyi ,kwa namna ya kipekee ya uongozi wake umeendelea kuchukua hatua madhubuti za kuimarisha ushiriki wa Wananchi wote katika maendeleo ya Taifa, ikiwemo Wanadiaspora wa Zanzibar waliopo nje ya nchi.

Aidha katibu mkuu ameeleza kuwa Serikali itaendelea kuwa karibu na wananchi wake walioko ughaibuni kwa kuweka mazingira wezeshi yatakayorahisisha upatikanaji wa fursa mbalimbali kwa wanadiaspora waliosajiliwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimatiafa na Uratibu wa Wazanzibar wanaoishi nje ya nchi (diapora) Dkt Haji  Gora Haji amesema kuwa Kwa sasa jumla ya Diaspora 1,312 tayari wamekamilisha usajili wao na  Ofisi inaendelea na utoaji wa elimu wa jinsi Diaspora wanaweza kujisali kupitia vyombo vya habari, mikutano na Diaspora kupitia jumuiya zao pamoja kusambaza taarifa katika mitandao mbalimbali

Related Articles