Waziri Dkt Saada Mkuya Salum ameongoza kikao cha Watendaji Wakuu na Maafisa kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Uratibu wa Diaspora Ikulu Zanzibar.

  • Dec 17, 2025
  • 2 Views

Waziri wa Nchi Afisi ya Rais - Ikulu Zanzibar Dkt Saada Mkuya akiongoza kikao cha Watendaji Wakuu na Maafisa  kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Uratibu wa Diaspora - Afisi ya Rais Ikulu na Kitengo cha Diaspora, Ushirikishwaji na Fursa - Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Tanzania.

Waziri Dkt Saada  alisema “Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaendelea kuimarisha Sera, Sheria na Mifumo itakayowezesha Diaspora kushiriki katika maeneo mbalimbali ya ujenzi wa Uchumi na maendeleo endelevu ya Zanzibar

aidha, katika kikao hicho, Katibu Mkuu Afisi ya Rais Ikulu Zanzibar Ndugu Saleh Juma Mussa alieleza kuwa “Lengo la kikao  ni kuongeza ushirikiano na kubuni njia sahihi za kuwafikia Diaspora ili waweze kurudi nyumbani na kuwa na tija katika nchi yao ya asili.

vile vile, Mkurugenzi wa Kitengo cha Diaspora, Ushirikishwaji na Fursa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ndugu Salvator Marcus Mbilinyi “Ameipongeza Serikali ya  Mapinduzi Zanzibar kwa kuandaa Sera na Sheria ya Diaspora na kupelekea kufanikisha utekelezaji wa shuguli za Diaspora kwa Zanzibar, pia alieleza mikakati ya kitengo cha Diaspora  kinavyofanyakazi.  ”.

Related Articles