Mke wa Rais wa Zanzibar mama Maryam Mwinyi ameuhakikishia umoja wa Asasi za kiraia za Marekani  kuwa zipo tayari kushirikiana na Asasi za kigeni kwa lengo la kuisaidia Serikali na kuwaletea maendeleo

  • Aug 13, 2022
  • 99 Views

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Zanzibar Maisha Bora Foundation na mke wa Rais wa Zanzibar mama Maryam Mwinyi ameuhakikishia umoja wa Asasi za kiraia za Marekani  kuwa zipo tayari kushirikiana na Asasi za kigeni kwa lengo la kuisaidia Serikali na kuwaletea maendeleo wananchi.Akifungua mkutano wa mashirikiano kati ya Asasi za Zanzibar na Marekani  mama Maryam amesema ushirikiano wa Asasi za kiraia kutasaidia kufikia malengo ya Serikali katika Katika kufikisha maendeleo kwa wnanchi.

Amesema ni vyema kwa Asasi za kiraia kuwa makini katika utendaji wake wa kazi ili kwenda sambamba na vipaumbele  vya Serikali .Amesema kuwa ushirikiano huo ni vyema ukaimarishwa kwani utazipa mwanga NGOs kiutendaji na kuwafikia walengwa. Hata hivyo Mama Maryam amesema Serikali itaendelea kujenga mashirikiano na Mataifa mbalimbali ili kuzijengia UWEZO na kutimiza MALENGO zilizojiwekea Asasi za kiraia za Zanzibar.

Mapema Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee  na Watoto Mhe. Riziki Pembe Juma amesema nguvu za Asasi za kiraia iwapo zitaendelea kupewa nguvu na uwezo basi Zanzibar itaweza kupiga hatua kimaendeleo .

Kwa upande wake Mrajis wa Asasi za kiraia Zanzibar ndugu Ahmed Khalid Abdullah na DK Rhonika Thomas wamepongeza juhudi zinazochukuliwa na Rais wa Zanzibar katika kuimarisha mashirikiano na Sekta binafsi  zikiwemo Asasi za kiraia za ndani na nje ya nchi.

Kipekee, Bi Adila Hilal Vuai - Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa kimataifa na Diaspora amemshukuru  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazanzibari wanaoishi nchini Marekani (ZADIA), Bwana Omar Haji Ali kwa jitihada zake za kuhakikisha wana Jumuiya hawo wamefika Zanzibar kwa lengo la kubadilishana mawazo na Uzoefu na Asasi za Kiraia. Vile vile Bi Adila Hilal Vuai ameendelea kuwasisitiza Diaspora kuendelea kuitangaza Zanzibar na Tanzania kwa Ujumla katika Mataifa walioyokuwepo kupitia Utalii na Uwekezaji. 

Mkutano huo umeandaliwa na Ofisi ya Rais-Ikulu kupitia Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Diaspora kwa kushirikiana Mrajis wa Asasi za kiraia Zanzibar kwa kushirikiana na Idara ya ushirikiano wa mambo ya nje pamoja na Wazanzibari wanaoishi nje ya nchi.

Related Articles