6th Tanzania Diaspora Conference 2019

  • Aug 03, 2018
  • 172 Views

Mgeni rasmi katika kongamano hilo ni Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Wahi sasa kufanya usajili

Not a member yet? Register now

DIASPORA KWA MAENDELEO, MTU KWAO NDIO NGAO!

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinapenda kuwatangazia wanadiaspora wote wa Tanzania pamoja na wananchi kuwa, kutakuwa na Kongamano la Tano la Diaspora Tanzania litakalofanyika siku ya Jumamosi na Jumapili ya tarehe 18 na 19 ya mwezi wa Agosti, 2018 katika Viwanja vya kufurahishia watoto vya ZSSF Tibirinzi, Wilaya ya Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba.

Mgeni rasmi katika kongamano hilo ni Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Wanadiaspora wote wenye ari na nia ya kushiriki wanapaswa kufanya usajili ama kwa kujaza fomu maalum zinazopatika katika ofisi za Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Uratibu wa Diaspora Zanzibar zilizopo karibu na Ikulu ya Mnazi Mmoja Unguja au wanapaswa kutembelea tovuti zifuatazo:-

  1. www.zanzibardiaspora.go.tz/diasporaconference2018/
  2. www.ompr.go.tz
  3. www.ikuluzanzibar.go.tz

Source: http://www.zanzibardiaspora.go.tz/diasporaconference2018/

Related Articles